Jumamosi 7 Februari 2026 - 08:02
Mapinduzi ya Kiislamu Iran, yameondoa udhalili kwa watu wa Iran/ Adui ameekeza katika vita vya kisaikolojia na uzushi

Hawza/ Khatibu wa Swala ya Ijumaa ya Qum amesema: Mapinduzi ya Kiislamu yameondoa udhalili kwa watu wa Iran na kuweka badala yake heshima na kumtegemea Mwenyezi Mungu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Sayyid Hashim Hosseini Bushehri katika khutba za Swala ya Ijumaa ya tarehe 6 February 2026 zilizofanyika katika Muswalla-ye Quds mjini Qum, huku akirejea maadhimisho ya mwaka wa arobaini na nane wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu alisema: Muongo wa Fajr wa Mapinduzi ya Kiislamu ulianza kwa kuwasili Imam Khomeini tarehe 12 Bahman. Wakati utawala wa kitwaghuti ulikuwa unatawala nchi, mapokezi makubwa yalifanyika kwa Imam marehemu. Siku ya tarehe 22 Bahman pia Imam Khomeini (r.a) kwa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu aliushangaza ulimwengu wa Mashariki na Magharibi.

Imamu wa Ijumaa wa Qum aliendelea kusema: Katika Mapinduzi ya Kiislamu kuna sifa ambazo zilisababisha mipango ya maadui kusambaratika. Pamoja na uadui wote walioufanya maadui, kwa bahati nzuri sifa hizi bado zinaendelea. Maadui waliifanya nchi yetu kuwa tegemezi na waliwadhalilisha wananchi, na maelfu ya washauri wa Marekani walikuwa wakitoa amri huku mfalme wa nchi akiwa hana taarifa.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisisitiza: Mapinduzi ya Kiislamu yaliondoa udhalili kwa watu wa Iran na kuweka badala yake heshima na kumtegemea Mwenyezi Mungu. Mapinduzi ya Kiislamu yaliwaingiza wananchi katika uwanja wa masuala ya kisiasa na kuwapa uwezo wa uchambuzi. Leo taifa la Iran ni miongoni mwa mataifa yenye uelewa mkubwa zaidi kuhusu masuala ya kisiasa, uchambuzi wa kisiasa na utambuzi wa adui.

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Maadui wamelitambua hili, ndio maana wakati mwingine huwateka vijana wa taifa katika mitego yao. Hawaitaki Iran yenye nguvu.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum alisema: Miaka 47 ya Mapinduzi ya Kiislamu haijapita kwa urahisi; miaka 8 ya vita vya kulazimishwa, jaribio la mapinduzi ya kijeshi, fitina za makundi na kadhalika ni miongoni mwa matukio ambayo Mapinduzi ya Kiislamu yamepitia, na kama kila moja ya haya yangetokea katika nchi nyingine, nchi hiyo isingebaki. Taifa la Iran pamoja na matatizo yote limeshikamana na mizizi, yaani mfumo wa Kiislamu.

Aliongeza kuwa: Hii haimaanishi kutokuwepo kwa matatizo, bali tumekabiliwa na changamoto kubwa na tumeweza kuzipita, na Mapinduzi ya Kiislamu bado yamesimama imara. Kongozi anang’aa kama jua, na adui anapomuona karibu na kaburi la Imam huingia katika mshangao na kutokuamini.

Imamu wa Ijumaa ya Qum alisema: Viongozi wanapaswa kujitahidi na kuzingatia miongozo ya Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi na kufanya kazi kwa juhudi maradufu. Aliendelea kuwa: Mtume Mtukufu (s.a.ww) amesema: “Bwana wangu ameniamuru kuwafanyia watu upole kama alivyoniamuru kutekeleza faradhi.”
Hapa kutekeleza faradhi na kuwafanyia watu upole kumewekwa pamoja.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi alisisitiza: Tunapaswa kufanya kazi ili wananchi wawe na furaha na wahisi kuwa tuko pamoja nao. Tunapaswa kuleta mabadiliko katika utendaji, tabia na maneno yetu ili wananchi wasikilize maneno yetu badala ya maneno ya wageni.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisema: Pamoja na kushinda changamoto na kulinda mwelekeo wetu, tumeweza kupata maendeleo mengi. Adui wakati mwingine huonesha hali kana kwamba hata watu waliokulia katika mazingira ya mapinduzi hawaoni maendeleo haya.

Imamu wa Ijumaa ya Qum aliongeza: Katika nyanja za kisayansi tumepiga hatua kubwa na tunalingana na nchi zilizoendelea. Kama alivyonena Imam Ali (a.s): “Elimu ni mamlaka.”
Kwa nguvu ya kisayansi tumeingia katika uwanja. Katika sekta ya anga, tiba, teknolojia za hali ya juu, mtandao wa kompyuta kubwa, satelaiti, dawa za kupambana na saratani na kadhalika, tuna wataalamu bora na maendeleo makubwa.

Alisisitiza kwamba; adui anajaribu kuwafanya wananchi wasiyaone maendeleo haya, na akaongeza: Nguvu ya vikosi vyetu vya ulinzi leo inazingatiwa na marafiki na maadui. Natumaini kwa fadhila za Mwenyezi Mungu mapinduzi haya yataendelea kubaki na kung’aa na tutashuhudia maendeleo zaidi yanayohusiana na Mapinduzi ya Kiislamu.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alikumbusha: Mapinduzi ya Kiislamu yameweza kuhamisha malengo ya Imam marehemu kwa vizazi vipya, na Inshaallah wachache walioathiriwa na wengine watarudi katika mkondo wa mapinduzi, na tutashuhudia umoja na mshikamano kama ule ulioshuhudiwa katika vita vya kulazimishwa vya siku 12.

Ayatullah Hosseini Bushehri alisema: Mwaka huu tumepitia njama mbili za adui, yaani vita vya kulazimishwa vya siku 12 na fitina za mwezi wa Dey, lakini Mapinduzi ya Kiislamu kwa fadhila za Mwenyezi Mungu yamesimama. Sisi tulipata madhara, lakini adui pia kwa fadhila za Mwenyezi Mungu atapata madhara makubwa. Tunaona fedheha ya viongozi wa Marekani na Ulaya ambao kwa miaka mingi walikuwa wakificha mambo, lakini kwa baraka za dua zenu wamepata kashfa ambayo hawana ujasiri wa kuinua vichwa mbele ya watu wao.

Khatibu wa Ijumaa ya Qum, akirejea tukio la watu tarehe 22 Dey, alisema: Wananchi waliunda tukio la kishindo, na tarehe 22 Bahman linapaswa kuundwa kwa nguvu zaidi na kwa utukufu mkubwa zaidi. Hatupaswi kumsahau Mwenyezi Mungu; maadamu tunashikamana na malengo ya kimungu hatuna huzuni, lakini viongozi wanapaswa kuwa makini zaidi kwani wajibu wao umeongezeka.

Aliendelea: Tarehe 22 Dey nyoyo zilikuja mitaani na tarehe 22 Bahman zikaunda utukufu mwingine, lakini viongozi wanapaswa kujali matatizo ya wananchi na ajira za vijana na kufanya kazi usiku na mchana.

Akizungumzia mazungumzo ya nyuklia alisema: Baadhi ya watu wana wasiwasi na kukosoa kuwa, kwa nini tufanye mazungumzo tena, kwa sababu hapo awali adui alitushambulia katikati ya mazungumzo hayo. Sisi, huku tukilinda masharti yetu na kuzingatia maslahi ya taifa, tulifanya mazungumzo ili kukamilisha hoja mbele ya ulimwengu.

Alisema: Ninauambia adui kwamba watu wetu ni wale wanaohudhuria popote panapohitajika, na hawataruhusu mgeni kuingia katika ardhi hii takatifu.

Akirejea kumbukumbu ya kiapo cha utiifu cha wanajeshi wa anga kwa Imam marehemu alisema: Wanajeshi wa anga tarehe 19 Bahman, katika siku ngumu za utawala wa kitwaghuti, walimpa Imam marehemu kiapo cha utiifu na kuvunja malengo yote ya adui. Maadui walidhani jeshi la anga ndilo lililokuwa la kuaminika zaidi kwao, lakini ilionekana kuwa nyoyo zao zilikuwa pamoja na Imam marehemu.

Imamu wa Ijumaa wa Qum alisema: Nawashukuru wananchi wa Qum na nchi nzima kwa kushiriki kwa wingi katika mji wa Karima Ahlul-Bayt (a.s) na Msikiti mtukufu wa Jamkaran katika nusu ya Shaaban. Jina la Imam Mahdi (a.f) linapaswa kubaki hai, na tawassul zetu zinapaswa kuongezeka. Kinachofanya usiku wa giza kuwa mchana pamoja na mipango yote ya adui si kitu kingine isipokuwa uangalizi wa Imam wa Zama (a.f).

Katika khutba ya kwanza alisema: Imam Ali (a.s) amesema:


“Yeyote anayeacha uchamungu huvutiwa na starehe na matamanio, huanguka katika upotovu wa maovu, na matokeo makubwa mabaya humkumba.”

Alisema: Migawanyiko, kuwepo kwa watu wenye nyoyo zenye maradhi katika safu za wapiganaji, jamii iliyoghafilika, ujinga, kutozingatia mwisho wa mambo na malengo ya kimungu, kukimbia kulipa gharama ya ushindi, kukiuka amri ya Imam wa jamii, na kuwepo kwa wasaliti katika jamii ni miongoni mwa sababu za kushindwa.

Imamu wa Ijumaa ya Qum alitaja uvumi na kuathiriwa nao kuwa sababu nyingine ya kushindwa na kusema: Mwenyezi Mungu katika aya ya 60 ya Suratul Ahzab anasema:

“Iwapo wanafiki na wale wenye maradhi katika nyoyo zao na wanaoeneza uvumi Madina hawataacha, tutakuchochea dhidi yao, kisha hawatakaa karibu nawe humo isipokuwa wachache.”

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisema: Athari mbaya ya uvumi ni kubwa kuliko mabomu na makombora, kwa sababu huandaa mazingira ya adui kutoa pigo la mwisho.

Alisema: Watu katika mawasiliano yao wakati mwingine kwa kutojali husambaza maneno ambayo hawana uhakika nayo, hata wakati mwingine kwa kusema kwamba mtu mwenye taarifa amesema, ili yafanye yakubalike. Wakati mwingine watu hawana nia mbaya bali hudhani wana habari mpya wanazopaswa kuwafikishia wengine.

Khatibu wa Ijumaa wa Qum aliongeza: Baada ya matukio ya hivi karibuni tumeona adui amewekeza katika vita vya kisaikolojia na uvumi katika masuala ya kijeshi, kisiasa, kitamaduni na kiusalama.

Alisema: Wananchi wetu wenye uelewa, hasa watu wa Qum ambao ni chimbuko la Mapinduzi ya Kiislamu, wanapaswa kuzingatia kwamba Mwenyezi Mungu katika aya ya 36 ya Suratul Isra anasema:
“Wala usifuate usiyokuwa na ujuzi nayo.”
Yaani msifuate habari na mambo msiyokuwa na yakini nayo mpaka myachunguze ili uvumi usiharibu mazingira ya jamii na nchi.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Walimu wa Hawza ya Qum alisema: Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume (s.a.ww) kuhusu waeneza uvumi awafukuze. Waeneza uvumi hawana silaha mikononi, lakini kwa ndimi zao huwafanya wale wasio na uelewa wa vyombo vya habari kuathirika.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha